Friday, January 21, 2011

Ligi Kuu ya Vodacom

Yanga 6 AFC 1
Ikicheza kwa maelewano na kujiamini, Yanga leo imeanza mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom kwa kishindo baada ya kufunga bila huruma AFC ya Arusha kwa jumla ya magoli 6 kwa 1.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Idd Mbaga dakika ya 23 ya mchezo, na baadae kidogo Nsajigwa akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 28 ya mchezo. Davis Mwape ambaye amesajiliwa hivi karibuni alidhihirisha kuwa yeye ni mfungaji baada ya kupachika goli safi dakika ya 43 ya mchezo. Hivyo hadi mapumziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa mabao 3 kwa bila.

Kipindi cha pili kilishuhudia Yanga ikiendeleza ubabe baada ya Mwape kufunga mabao mawili, huku Mbaga, mshambuliaji chipukizi ambaye anaonekana michuano ya mapinduzi imemjenga, akiongeza bao lingine, kuhitimisha magoli karamu ya magoli 6.

Source: YANGA

.

7 comments:

Anonymous said...

jamani mupo wale mafara?tumeanza sasa.

Anonymous said...

Kama kawaida ya YeboYebo huwa anaanza kwa mkwala ila mwishoni huwa anakubali yaishe!!! Yaani mmemfunga maiti mnachonga?? ama kweli KIPOFU AKIONA MWEZI MATAKO HULIA MBWATA

Anonymous said...

yaani wewe faara kweli brazil imeshindwa kwenda>

Anonymous said...

waende brazil na koni alambe nani?

Anonymous said...

yule faara wa simba yu wapi? unaomboleza?

Unknown said...

Hawezi kusema tena kwani anaogopa Boko na Ngassa watasikia tambo zake feki.

SHIKABWE MSAFIRI said...

VISHUKA VYA SIMBA VIMEDONDOKA,ETI OO AZAM NI JAMAA ZEETU,KWANI WAO HAWAOGOPI KUSHUKA DARAJA,HALAFU MAKOCHA WA KIZUNGU HAWATAKI LONGOLONGO WANATAKA KAZI,CHEZENI MPIRA ACHENI MANENO LAZIMA SIMBA MTASHINDA,PIA NAKUFUNGWA NA KUTOA SULUHU LAZIMA HAMUWEZI KUKWEPA HAYA,JITUMENI SANA.