Tuesday, February 15, 2011

Manji ang'oka?

MDHAMINI wa Yanga, ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji amedaiwa
kujiondoa katika klabu hiyo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilizopatikana Dar es Salaam zimedai Manji ameamua kujiondoa ili kupumzisha afya yake baada ya kuchoshwa na kelele za baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na pia ubadhirifu wa fedha za klabu kwa baadhi ya viongozi.

Kwa takriban mwezi sasa kumekuwa na mgogoro ndani ya Yanga ukihusisha baadhi ya viongozi na wanachama na wakati mwingine baadhi ya viongozi kwa viongozi.

Wiki iliyopita baadhi ya wanachama wa tawi la Yanga Tandale Kwa Mtogole walimtaka mfadhili huyo aondoke Yanga kwa madai anaivuruga klabu yao.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kilichomfanya mdhamini huyo kujiondoa Yanga ni namna klabu hiyo isivyoendeshwa kwa mpangilio na kwamba fedha nyingi zinatoka lakini hazionekani
zinatumika vipi.

“Yanga kuna ubadhirifu unafanyika ndio maana Manji amekuwa akipiga kelele kila siku ufanyike ukaguzi ili wanachama wanaosema anaivuruga klabu waone nani ni mvurugaji,”kilisema chanzo hicho.

Source:HABARI LEO

10 comments:

Anonymous said...

poa sana mtazamo wangu ulikua unabeba maji katika gunia, ulikua unategemea nini??????? pesa unayo anzisha shule ya mpira uone pesa zako zinavyotumika
mdau wa kweli yanga.

Anonymous said...

kweli manji ulikua na nia njema kabisa ila waswahili wakiona hawapati chochote ni kuharibia wengine .manji yanga will miss you! haya sasa tuone wangapi wanakuja kuisaidia yanga.

Anonymous said...

MANJI UMEONA ? WATU HAWANA SHUKHRANI KABISA .ULI WIMBO NAUKUMBUKA WATU WA SIKU HIZI MARIDADI SANA MARIDADI SANA LAKINI MFUKONI HAMNA KITU.

Anonymous said...

MANJI UMEONA ? WATU HAWANA SHUKHRANI KABISA .ULI WIMBO NAUKUMBUKA WATU WA SIKU HIZI MARIDADI SANA MARIDADI SANA LAKINI MFUKONI HAMNA KITU.

Anonymous said...

kagera 1[mwaikimba]yanga 0,pambano linaendelea ,yanga wanashambulia kama nyuki wamekataliwa mabao mawili offside

Anonymous said...

Mtamkumbuka Papic,

Anonymous said...

Si mlimtaka Minziro, sasa hayo ndo matunda ha ha ha

Anonymous said...

hizi fisi hazina adabu kabisa.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___