Monday, February 28, 2011

Yanga kurejea kileleni leo?
Yanga ikiwa chini ya Sam Timbe leo ina nafasi nyingine ya kurejea kileleni mwa Ligi Kuu endapo itaishinda Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Timbe ana kibarua cha kuhakikisha timu yake inarudi kileleni itakapovaa wanajeshi hao huku wakifahamu kuwa ushindi utawarejesha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Yanga yenye pointi 35 sawa na Azam ina mchezo mmoja pungufu ya vijana hao wa lambalamba ambao wamekuwa wakiongoza hadi jana kabla ya mechi baina ya Simba na Mtibwa Sugar ambayo Simba iliibuka mshindi kwa mabao 4-1.

Hata hivyo, Yanga leo itacheza mchezo huo huku ikiwa inahitaji ushindi wowote ili kukaa tena kileleni, lakini mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na kuwa viwango tofauti.

Ruvu Shooting ina pointi 15 baada ya kucheza michezo 16 ikiwa katika nafasi ya tisa inatafuta pointi tatu ili kujiepusha na hatari ya ya kushuka daraja wakati Yanga inataka kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Katika mchezo huo, Yanga inaweza kutomtumia kipa wake tegemeo, Yaw Berko kutokana na kuwa na kadi mbili za njano, hali ambayo imekuwa ikimtia wasiwasi kochaTimbe.

Kama Timbe atamchezesha Berko na pengine kupata kadi nyingine , basi kipa huyo ataukosa mchezo mwingine dhidi ya watani wao wa jadi ,Simba Jumapili.

8 comments:

Anonymous said...

Jamaa mkipata habari mtujulishe siye tulio mbali na nyumbani tz

Anonymous said...

matokeo bado hamjapata?

Anonymous said...

Huyu jamaa Simba, msimwami kabisa, Yanga kashinda bao 1 lilofungwa na Jerry Tegete

Anonymous said...

tunamjua sana halafu anajifanya mpole ,kweli fisi ni fisi tuuu,.

Anonymous said...

watu wengine damu hawana kabisa yaani we unaongopa mbinguni nawa tu wapo chini huoni kuwa kazi unayo halafu unataka tuombe dua we mwenyewe mnyama

Anonymous said...

Haiwezekani yanga hawana uwezo wa kushinda

Unknown said...

Ni kweli kabisa, haiwezekani Yanga kutokuwa na uwezo wa kushinda. Kwa vyovyote ulimaanisha hivyo ila kwa bahati mbaya hujui kiswahili.

Anonymous said...

Hebu rudi shule kabla hujaingilia "blogs" za walopevuka ukajifunze matumizi ya alama za mkato, nukta, nk. Alichosema excomta hapo juu ni sahihi. kwa kutotumia alama zilizotajwa ipasavyo maana alokusudia mchangiaji alotangulia kabla ya excomta imebadilika. Najua huyo ni mnyama alikuwa na lengo la kuidhihaki Yanga, lakini kwa kutojua kwake kiswahili kajikuta anaisifia. POLE SANA.