Thursday, April 07, 2011

Yanga 3 African Lyon 1
Hatimaye Yanga leo imeifikia timu ya Simba kwa pointi baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika hivi punde.

Ushindi huo unaifanya Yanga kujikusanyia pointi 46 sawa na Simba huku Yanga ikiwa na tofauti ya magoli (Goal Difference) ya 22 wakati Simba ina 21.

Kwa hali hii, michezo ya mwisho ya ligi kwa timu hizi mbili itakuwa ya umuhimu mkubwa kwani ndizo zitakazoamua bingwa wa ligi hiyo. Yanga itakwaana na Toto Africa Jijini Mwanza wakati Simba itaikaribisha Majimaji Jijini Dar.

Magoli katika mchezo wa leo yalifungwa na Iddi Mbaga aliyefunga mabao mawili pamoja na Davis Mwape. Goli la kufutia machozi la Lyon lilifungwa na beki wa Yanga Chacha Marwa katika harakati za kuokoa.

Tusubiri Jumapili kama ubingwa utatua Jangwani au Msimbazi.

8 comments:

Anonymous said...

CM umenichanganya kidogo, msimamo wa Ligi unaonyesha Simba katuzidi magoli ya kufunga...labda unieleweshe hizo Goal difference unazosema...Nitashukuru.

Mdau
Italy

CM said...

Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya magoli 22. Imefunga magoli 29 na kufungwa 7. Goal difference hapo ni (29-7 = 22).

Simba imefunga magoli 36 na kufungwa 15. Gosl difference hapo ni (36-15 =21)

Yanga ina GD ya 22, Simba ina 21

Anonymous said...

Jamaa matokeo bado hayajapatikana tulio mbali mioyo inaenda mbio tujulisheni mlio na habari

CM said...

Yanga Bingwa mpya wa soka wa Tz baada ya kuichapa Toto 3-0

Simba nayo imeichapa Majimaji 4-1

Anonymous said...

cm ahsante hongera wana yanga kwa kurudisha ubingwa wenu kila la kheri sasa viongozi jipangeni upya mtizame wachezaji mnaowahitaji mapema

Anonymous said...

Mashabiki wa Yanga tusihofu kwani msimu ujao tutachukua ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya 24...hii inatokana na usajili ulivyofanyika kwa ustadi mkubwa.

Anonymous said...

Mimi pamoja na mashabiki wenzangu tuliopo Usangi tunapenda kuushukuru uongozi wa Yanga pamoja na benchi la ufundi kwa kuhakikisha tunashiriki kagame cup....ni mimi shabiki sugu{Fanuel Gasper...0714359690}.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___