Thursday, February 15, 2007

Mwalala aelekea Sweden


Mshambuliaji nguli wa Yanga na Harambee Stars, Ben Mwalala ameondoka Jijini Dar es Salaam juzi kuelekea nchini Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu moja nchini humo.

Mwalala ambaye mwezi uliopita aliibuka mmoja wa wafungaji bora katika michuano ya Kagame anakuwa Mkenya wa pili kuondoka msimu huu baada ya mchezaji mwingine John Barasa naye kutimkia Indonesia kwa ajili ya majaribio ya soka la kulipwa.No comments: