Monday, February 19, 2007

Yanga sasa shwari


Makundi matatu yaliyokuwa yakipingana ndani ya Klabu ya Yanga - Yanga Asili, Yanga Kampuni na Yanga Asili kwa kauli moja wamepitisha rasimu ya muafaka ambayo imeinusuru klabu hiyo kutoka kwenye mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka saba.
Miongoni mwa mambo ambayo yapo kwenye muafaka, makundi yote matatu yatanunuliwa hisa na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuf Manji. Kwa kuanzia, kila mmoja atanunuliwa hisa za sh 10,000.

Kwa kiasi hicho, Manji atagharamia kiasi cha sh mil. 60 kutokana na klabu hiyo kwa sasa kuwa na wanachama 6,000 kwa pande zote tatu.

Katika mgawanyo huo wa hisa, upande wa klabu umebaki na asilimia 51.

Kuhusu mgawanyo wa asilimia 49, asilimia 51 zitanunuliwa na wanachama huku asilimia 49, zitauzwa kwa umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, baada ya mchakato huo, Yanga inataraji kupata sh bil 3.

No comments: