Wednesday, February 21, 2007

Ni Young Africans Sports Corporation Limited!!!!!!!

Klabu ya soka ya Yanga imebainisha kwamba jina jipya la kampuni iliyopitishwa kuanzishwa ni Young Africans Sports Corporation Limited.

Akifafanua kuhusu kampuni hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Yanga Bw. Francis Mponjoli Kifukwe alisema awali Young Africans Sports Club Limited ndiyo ilikuwa imesajiliwa mwaka 2000 na kilichofanyika hivi majuzi ni mabadiliko tu ya jina.

Hivi karibuni, makundi matatu ya Yanga Asili, Kampuni na Academia yaliungana kuwa kitu kimoja na kukubaliana kufanya usajili wa kampuni ya umma na kuahidi kulimaliza suala hilo kwa kipindi cha wiki mbili.

Wanachama wa Yanga pia walipitisha mapendekezo ya mchakato wa kuuzwa kwa hisa za
kampuni hiyo na kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi ujao. Kwa sasa, timu ya Yanga ipo Zanzibar kujiandaa na mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Athletico ya Angola itakayofanyika Machi 3, jijini Dar es Salaam.

No comments: