Thursday, March 15, 2007

Kikosi chetu sasa kipo ndani ya Angola


Kikosi kizima cha Yanga ambacho kilikuwa nchini Afika ya Kusini kwa mazoezi, kimeelekea Luanda Angola kwa ajili ya pambano la marudiano la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Petro du Luanda hapo Jumapili.

Yanga ambayo awali ilikuwa iondoke Ijumaa, imelazimika kuondoka mapema kufuatia ndege waliyokuwa wamepanga kuondoka nayo hapo awali kufutwa.

Ikiwa huko Sauzi, Yanga ilicheza mechi 3 za kujipima nguvu. Ilicheza dhidi ya Pretoria FC na kushinda 2-0, ilifungwa na Luz 2-1 na kutoka sare na Supersport United 1-1.

Wakati huo huo wapinzani wa Yanga katika mchezo huo timu ya Petro du Luanda wamefungwa 2-0 na Santos FC katika mchezo wa ligi kuu ya huko Luanda.

3 comments:

Anonymous said...

Hewalaa!
Ebwana tuwekee LOGO ya yanga humu ndani na pia mapicha ya wachezaji na wasifu wao. Itakuwa safi sana na muda si mrefu itabidi tuanzishe URL ya yanga.
MUNGU IBARIKI YANGA NA TZ KWA UJUMLA.

CM said...

Ninashukuru kwa mawazo mazuri "anony" hapo juu. Nitajitahidi kufuata ushauri wako, japokuwa sina picha za wachezaji wote.

Ila kama unataka maelezo zaidi kuhusu kikosi cha sasa cha Yanga, nimejitahidi kuchangia kwenye http://en.wikipedia.org/wiki/Young_Africans_FC

MTANZANIA. said...

Mc, nimeipenda blog yako. Naomba tuwasiliane. Karibu pia nyumbani kwangu.