Wednesday, March 14, 2007

Yanga, Supersport Utd sare

Yanga imetoka sare ya 1-1 na Supersport United ya Afrika ya Kusini. Mabao yote yalifungwa katika kipindi cha pili, bao la Yanga lilifungwa na Said Maulid SMG wkati lile la Supersport United lilifungwa dakika 7 kabla ya mpira kumalizika.

Juzi usiku kikosi cha wachezaji wa akiba wa Yanga kilifungwa mabao 2-1 na Luz ya Angola katika mchezo mwingine wa kirafiki.

No comments: