Tuesday, March 13, 2007

Mechi ya Supersport na Yanga yaahirishwa

Ule mpambano wa kujipima nguvu kati ya Yanga na Supersport United uliokuwa ufanyike jana, umeahirishwa na badala yake mtanange huo utasukumizwa leo.

Pambano hilo limeahirishwa kutokana na timu ya Supersport Utd kuwa kwenye hali ya uchovu wa safari ambapo walikuwa jijini Cape Town kupepetana na Ajax ya huko katika mchezo wa ligi ya nchi hiyo.

Jana usiku Yanga ililazimika kubadili ratiba na kuamua kucheza na Luz ya Angola katika mchezo mwingine wa kirafiki.

1 comment:

Anonymous said...

Yanga sasa inatisha kama Rift valley.