Monday, March 12, 2007

Leo ni Supersport United FC vs Yanga

Baada ya kuitungua Pretoria FC kwa mabao 2-0 mwishoni mwa wiki, leo Yanga inaingia tena uwanjani dhidi ya timu ngumu ya Supersport United FC katika mchezo wa kujipima nguvu.

Supersport ambayo ipo katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Afrika ya Kusini kama itachezesha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza, basi itamkutanisha kipa wake Denis Onyango na Yanga. Ikumbukwe kwamba Onyango aliwahi kutua Dar kwa ajili ya kusaini kuichezea Yanga lakini mazungumzo hayakufikia muafaka.

Katika mchezo wa Jumamosi, mabao ya Yanga yalifungwa na Credo Mwaipopo na Hussein Swedi.

MAPAMBANO YANAENDELEA.

1 comment:

Zaida said...

Well written article.