Saturday, March 10, 2007

PROGRAMU YA YANGA NDANI YA SAUZI HII HAPA:

Kocha Mkuu wa Yanga Micho ameandaa programu kabambe kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Petro Athletico du Luanda.

Yanga ambayo imefikia Cross Media Training Center, leo asubuhi itakuwa na mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Pretoria FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

Jumatatu asubuhi watacheza mechi nyingine na Supersport FC.

Jumanne usiku watakabiliana na timu ya Luz kutoka Angola.

Jumatano aubuhi ndipo Kocha Micho atakapofanya uteuzi wa wachezaji 18 watakaokwenda Angola kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Petro du Luanda.

Kwa undani zaidi click picha hapo juu.

Bila shaka Programu itakwenda sawa bin sawia, ALUTA CONTINUA!!!!!!!

No comments: