Friday, March 09, 2007

SMG yaelekea Sauzi


Winga mwenye kasi wa Yanga Said Maulidi "SMG" anatarajia kuondoka nchini leo mchana kuungana na wenzake wa kikosi hicho huko Afrika ya Kusini.

SMG, Lulanga Mapunda na Athumani Iddi hawakuondoka juzi na wenzao kwa sababu mbalimbali. SMG hakujiunga na wenzake kutokana na kuuguliwa na mtoto wake, Lulanga Mapunda anatumikia adhabu ya TFF ya kutocheza soka miezi 6. Athumani Iddi pasi yake inashikiliwa na TFF ambayo inamtambua kama mchezaji wa Simba.

Safari njema SMG!!!!!!!

No comments: