Saturday, March 17, 2007

Shadrack Nsajigwa "Fuso"


Ivo Mapunda - Tz 1


Pamoja na kuwekwa kwenye kambi ya zamani ya jeshi, Yanga kesho inatarajia kumaliza hasira zake dhidi ya Petro du Luanda katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika huko Luanda.

Wenyeji wa mechi hiyo wameiweka Yanga kwenye kambi ya zamani ya Jeshi ambayo ipo km zaidi ya 20 kutoka kwenye uwanja waliopangiwa kufanyia mazoezi.

Katika hatua nyingine, inasemekana kwamba viongozi wa Petro du Luanda wamewafuata waamuzi wa mchezo huo kutoka Zimbabwe na kutua nao huko Luanda. Kazi kweli wanayo hawa ndugu zetu.

Hata hivyo pamoja na visa vyote hivyo sisi wana Yanga siku zote tunaamini kwamba hivyo ni visa tu ambavyo mwisho wake itakuwa ni Yanga kusonga mbele. Tuna kikosi kizuri tu ambacho kinaundwa na nyota kama akina kipa Ivo Mapunda, beki wa kulia Shadrack Nsajigwa, mshambuliaji SMG n.k

Kila la heri Yanga. Mungu Ibariki Yanga Daima!!!!!!!3 comments:

Anonymous said...

Una habari Yanga kapigwa goli mbili kwa dundu, lakini anandelea refa alikuwa anawaonea kiasi Micho akachukizwa mpaka kupigwa red card

Anonymous said...

Duh, si mbaya ili mradi tunasonga mbele.

CM said...

Mola hamtupi mja wake