Monday, March 19, 2007

Yanga twende kazi!!!!!!!!

Ule msemo kwamba Fitina yako ni bahati kwangu ulidhihirika jana huko Luanda Angola baada ya mashujaa wetu Yanga kusonga mbele licha ya kufungwa 2-0.

Kipigo hicho hakikuitosha Petro du Luanda kusonga mbele kwani ilihitaji ushindi wa mabao 4-0. Hadi mapumziko mabao yalikuwa 0-0. Kwa matokeo hayo Yanga imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 kufuatia ushindi wa 3-0 walioupata nyumbani wiki mbili zilizopita.

Petro du Luanda ilionekana wazi kubebwa na mwamuzi wa mchezo huo kutoka Zimbabwe ilinyimwa penalti katika kipindi cha kwanza baada ya SMG kuangushwa ndani ya eneo la 18. Kutokana na hali hiyo, daktari wa timu ya Yanga alimlalamikia mwamuzi na hapo hapo daktari wa timu alipewa kadi nyekundu.

Katika kipindi cha pili Yanga ilifungwa mabao katika dakika za 75 na 90 huku kocha wa Yanga Micho akilimwa kadi nyekundu kwa kumlalamikia mwamuzi huyo kutoka Zimbabwe.

Katika mchezo huo Yanga iliwakilishwa na: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Wisdom Ndhlovu, Edwin Mukenya, Hamis Yusuf, Waziri Mahadhi, James Chilapondwa, Amri Kiemba/Credo Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Said Maulid na Abdi Kassim.

Kwa ushindi huo Yanga sasa itakutana na Esperance ya Tunisia tarehe 6 Aprili huko Tunis na timu hizo zitarudiana Aprili 21 au 22.

SISI SASA TWASONGA MBELE PAMOJA NA FITINA ZOTE ZA WAANGOLA, FITINA ZAO NI BAHATI YETU. ALUTA CONTINUA, HONGERA SANA KWA WADAU WOTE!!!!!!!!!

4 comments:

Anonymous said...

EBU WEKA HABARI YA ATHUMANI IDD TUCHANGIE PLEASE

Anonymous said...

Swala la Idd Athuman, si la kutatanisha kama inavyoongelewa bali ni ubabaishaji wa viongozi wa soka kwa sababu sheria za FIFA ziko wazi mchezaji anaweza kuvunja mkataba kama mambo si kama alivyotazamia au anaweza kuunua mkataba wake. sasa huyu kijana anaonewa kwa sababu ya unazi uliopo kwenye vyombo vyetu. Yanga wakikata apeal FIFA yote yatawekwa hadharani

Anonymous said...

Haloo wewe jamaa.

Hizi stori unazobandika hapa ninajua kwamba umeziiba kutoka katika gazeti fulani la kila wiki na hutaki kueleza kwamba si za kwako na wala wale unaowaibia hukuwataja.

Nikiwa mmoja wa wadau wa gazeti hilo nakusihi uwe unatutaja gazeti letu vinginevyo tutakufikisha mbele ya sheria.

Huu ni wizi laivu na hauruhusiwi kabisa kwa mujibu wa miongozo ya kamisheni yetu ya blogu nchini. Kuwa makini acha wizi.

Anonymous said...

Wee anonimous hapo juu acha hizo... wewe simba nini.. au umetumwa? CM hajaiba kitu, hapa anaweka habari kwenye blog yake na hii haimzuii mwenye gazeti kuuza, wala wewe hulipii kusoma hapa.

CM, hebu tupe habari zingine motomoto ya chama letu, maana tumekuwa kimya toka Monday. Waache watani wetu wabaki na kocha wao wa makipa..