Monday, March 26, 2007


Mmisri kuchezesha mechi ya Yanga na Esperance


Mwamuzi Esam Abd El Fatah kutoka Misri atakuwa mwamuzi wa kati katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Klabu bingwa Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye mtandao wa Shirikisho la soka Afrika CAF, El Fatah atasaidiwa na Abdel Nabi Nasser Sadek pamoja na Abou Elela Ahmed Said kutoka Misri.

Mwamuzi El Fatah alikuwa mmoja wa waamuzi wachache kutoka Afrika waliochezesha fainali za Kombe la Dunia 2006 huko Ujerumani. Mechi pekee aliyochezesha ilikuwa kati ya Japan na
Australia.

Mwamuzi ndiyo huyo, tuombe Mungu hiyo tarehe 6 Aprili 2007 mambo yanyooke.

2 comments:

Anonymous said...

Inshahlaah,

Mungu yupo nasi,

Nalitolela, P. S. said...

sitaki kuwa persimist, lakini haya mambo ya kucheza na mwarabu na refa kuwa mwarabu yashatuumiza nyuma.

Ni mambo ya KESI YA NYANI UNAMPELEKEA NGEDERE AAMUE

I know El Fatah is a ref with International recognition, lakini....

anyways, ngoja tuone. Mungu mkubwa.