Thursday, March 22, 2007


Athumani Iddi

Wachezaji 11 wa kikosi chetu wameitwa na mataifa yao kwa ajili ya mechi za kutafuta nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika Ghana mwakani.

Kwa upande wa Tanzania - Taifa Stars ambayo itakwaana na Senegal Jumamosi wachezaji 8 walio katika timu hiyo ni Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Amri Maftah, Abdi Kassim, Saidi Maulid, Gaudence Mwaikimba, Hamisi Yusuf na Ndir Haroub. Naye Atumani Iddi - mchezaji mtarajiwa wa Yanga yupo Senegal.

Edwin Mukenya ameitwa na timu yake ya Taifa ya Kenya - Harambee Stars kwa ajili ya pambano la timu hiyo dhidi ya Swaziland.

Kwa upande wa Malawi - The Flames wachezaji James Chilapondwa na Wisdom Ndhlovu wameitwa kujiunga na kikosi cha timu hiyo ambacho kitacheza mchezo mmoja wa kirafiki. The Flames wanajiweka sawa baada ya kupata kocha mpya Steven Constantine kutoka Uingereza.

Kila la heri wana Yanga popote mlipo.

No comments: