Monday, March 05, 2007

VIVA YANGA!!!!!!!!!!!!!!

Mabingwa wa Tz Yanga jana walifanya kile ambacho watu wanapenda baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Petro Athletico ya Angola katika pambano la Ligi ya mabingwa ya Afrika iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo ulichagizwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko yaliyofanywa na Kocha wa Yanga, Sredjovic "Micho" kwa kumwingiza Mrisho Ngassa ambaye alileta uhai mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri kwa timu zote, na Yanga ilishindwa kabisa kuelewana hasa mshambuliaji wake Gaudence Mwaikimba alikuwa akipoteza mipira mingi.

Katika kipindi cha pili Yanga ilipata bao la kwanza katika dakika ya 77 kupitia kwa beki wa Athletico Renato aliyejifunga kwa kichwa akiwa katika harakati za kuokoa krosi ya Shadrack Nsajigwa.

Bao la pili ktk dk ya 82 ambalo lilikuwa zuri zaidi lilifungwa na Abdi Kassim kwa kiki kali ya chini chini kufuatia krosi iliyotoka kwa Shadrack Nsajigwa.

Mrisho Ngassa aliipatia Yanga bao la tatu katika dk ya 87 baada ya kupokea mpira wa kurushwa kutoka kwa Amri Kiemba.

Katika mchezo wa jana, Yanga iliwakilishwa na: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Wisdom Ndlovu, Hamis Yusuf, Nadir Haroub/Amri Kiemba, Edwin Mukenya, James Chilapondwa/Mrisho Ngassa, Waziri Mahadh, Gaudence Mwaikimba/Thomas Maurice, Said Maulid na Abdi Kassim.

Kwa ushindi huo, Petro Athletico inahitaji ushindi wa mabao 4-0 katika mechi ya marudiano huko Luanda wiki mbili zijazo.

VIVA YANGA, MAPAMBANO YANAENDELEA!!!!!!!!

4 comments:

Anonymous said...

Hongereni saana Yanga. Ama kweli jana muziki ulikuwa mzito kwa waangola. Nawatakia kila la kheri wiki 2 zijazo...

Anonymous said...

HOngereni sana Yanga.Hadi Gatuso kapata habari zenu huku Milano!CIAO!

Anonymous said...

Aminiya baba kwa hii site!!

CM said...

Aminia sasa hivi ni kicheko tu mtaani.