Friday, April 27, 2007

Athumani Iddi aanza kuona mwanga wa ukombozi

Shirikisho la soka nchini TFF limeipa Simba mwezi 1 ktafuta msuluhishi wa mgogoro wa mkataba wake na mchezaji wake ambaye hivi sasa anataka kuhamia Yanga - Athumani Iddi.

Simba iliingia mkataba wa miaka 3 na Athumani Iddi lakini mchezaji huyo akaamua kusaini katika fomu za Yanga kwa madai kwamba Simba haijamtekelezea mambo kadhaa ambayo yapo katika mkataba wake.

Moja ya vipengele vya mkataba huo unaruhusu kuvunjika kwa mkataba kwa kutumia wasuluhishi ambapo tayari Atumani Iddi ameteua mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria nchini asimamie suala hilo lakini Simba katika hali ya kutaka kumkomoa Iddi, haitaki kuvunja mkataba na katika hali isiyoeleweka wanachama wamepiga kura kuzuia uongozi kuendelea na taratibu za kushughulikia suala la kuvunja mkataba.

Athumani Iddi hayupo tayari kuchezea Simba msimu huu, lakini viongozi wa Simba bado wanamng'ang'ania. Sijui ni kwa faida ya nani? Ni vizuri kwa TFF kuingilia kati suala hili ambalo viongozi wa Simba wameshindwa kutumia busara.

Wadau mnasemaje kuhusu suala la Athumani Iddi? Kazi kwenu.

1 comment:

Anonymous said...

Kwa mara ya kwanza viongozi wa TFF wameamua ku-think rationally kuhusu hili suala.

Mkataba wowote halali unakuwa na milango miwili, wa kuingilia na kutokea, na pande zote mbili za mkataba zinakuwa na haki sawa kwenye kutumia hiyo milango.

Sasa Athumani Idd hakutimiziwa vipengele vya mkataba, kitu ambacho kinafanya mkataba uvunjike automatically, because of frustration of one party by the other.

Tunaambiwa na watu wa ndani ya simba (kocha Elias aliyetua msimbazi kwa mbwembwe nyingi saana..) kuwa viongozi wa simba wana uwezo mdogo (wa kufikiria.. na kuongoza..) pengine ndio maana wanashindwa kuelewa jambo dogo kama hili.

Tuombe suala hili liishe ndani ya huu mwezi ili kijana aongeze nguvu kwenye timu. Akiingia kwenye kiungo bila shaka baadhi ya viungo kama James Chilapondwa wataenda mbele kuongeza nguvu kwenye mashambulizi...