Friday, April 20, 2007

Kama tutatoka......ni kwa Waarabu tena!!!!!!!!


Shirikisho la Soka la Afrika CAF limetoa ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Raundi ya 4 ambapo timu zilizoshindwa kwenye raundi ya 3 ya Klabu Bingwa Afrika zitaingizwa kwenye kombe hilo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, timu itakayoshindwa katika mechi kati ya Yanga na Esperance itachuana na mshindi kati ya Assosiation Sportive Olympique de Chlef (ASO Chlef) ya Algeria dhidi ya Al Merreikh ya Sudan. Timu hizo mbili zinatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano huko Sudan kesho huku ASO Chlef tayari ikijivunia ushindi iliopata nyumbani wa 1-0.

Mechi hizo za raundi ya 4 ya Kombe la Shirikisho zinatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 4-6 Mei na marudiano yatakuwa tarehe 18-20 Mei.

Lakini kwanza tusifikirie hayo, bila shaka watakutana na Esperance kwa vile sisi matumaini yetu ni kuendelea na Ligi ya Mabingwa.

5 comments:

Anonymous said...

hivi tumekumbuka mazoezi ya penati?

Anonymous said...

Japokuwa hatuna rekodi nzuri kwa matuta lakini hata ile timu iliyokuwa inasifika Tz kwa matuta - Simba ilichemsha kwa Textile de Pungue.

Mungu Ibariki TZ.

Anonymous said...

Nadhani watakuwa wamekumbuka. Sasa benchi la ufundi liko imara, majuzi nilishuhudia benchi pakiwa hapatoshi pale Sheikh Amri Abeid, AFC alipolala 5-0,.. Micho, Rade na Siwa... mmoja wao bila shaka atakuwa amekumbushia hilo.

Munu Ibariki YAfrica, na Tanzania..

Anonymous said...

Mimi ni Yanga damu. Lakini miaka ya hivi karibuni upenzi umepungua. Nilikatishwa tamaa baada ya kuona naumiza roho bure kwa kuwa mshika bango huku timu ikiniangusha.

Blogu yako imenifanya nipate tena mwamko wa kufuatilia masuala ya timu yangu.

CM said...

Karibu sana bwana Ndesanjo. Nyie wakongwe wa blog ndiyo mmetuonyesha njia. Nakushukuru wewe pamoja na wanablog wote kwa kuendelea kutembelea blog hii yetu sisi wana Yanga.