Monday, April 02, 2007

Micho afungiwa na CAF


Shirikisho la soka Afrika CAF limewafungia kwa mechi moja Kocha Milutin Sredjovic 'Micho" na meneja wa timu ya Yanga Robert Ekerege kwa utovu wa nidhamu.

CAF inadai kwamba wadau hao wa Yanga walifanya utovu wa nidhamu katika mechi ya marudiano dhidi ya Petro Athletico huko Luanda ambapo Yanga ilifungwa 2-0.

Katika mechi hiyo, Micho na daktari wa timu Dk. Sufiani walipewa kadi nyekundu lakini cha kushangaza Ekerege naye amehusishwa kwenye adhabu hiyo wakati Dk. Sufiani ameachwa bila adhabu yeyote.

Dk. Sufiani alipewa kadi nyekundu kwa kumlaumu mwamuzi kwa kutotoa penalti baada ya Said Maulidi kuangushwa kwenye eneo la hatari. Micho alipewa kadi nyekundu kwa kosa la 'kumsahihisha' mwamuzi wa akiba ambaye alikosea kuonyesha namba ya mchezaji anayetakiwa kutoka wakati Yanga wanafanya mabadiliko.

Hata hivyo Micho alihisi kuwa kutakuwa na adhabu kama hiyo na kwa wiki moja sasa amekuwa akiifundisha Yanga akisaidiwa na Mserbia mwenzake Rade Dragojevic ambaye ndiye atakuwa kwenye benchi la ufundi siku ya pambano dhidi ya Esperance Ijumaa ijayo.

Tutasonga tu hakuna noma, dawa ni kujipanga tu.

1 comment:

Anonymous said...

Hi, very interesting post, greetings from Greece!