Monday, April 23, 2007

Ni Al Merreikh

Klabu kongwe ya Al Merreikh (au El Merreikh) ya Omduran, Sudan ndiyo wapinzani wetu katika mechi ya Raundi ya 4 ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Al Mereikh imeingia katika raundi hiyo baada ya kuitoa ASO Chlef ya Algeria kwa jumla ya mabao 3-1 (ilifungwa 1-0 ugenini na kushinda 3-0 nyumbani). Hapo awali kwenye raundi ya pili Al Merreikh iliitoa AS Cotton ya Chad kwa jumla ya 5-2 (ilifungwa 2-0 ugenini na kushinda 5-0 nyumbani)

Kwa haraka haraka ukiangalia takwimu za timu hiyo, utaona timu hiyo si nzuri sana inapokuwa ugenini lakini inapokuwa nyumbani huwa inatumia vizuri sana mechi zake za nyumbani ambapo hadi sasa haijafungwa goli na imepata mabao 8 katika mechi mbili. Kwa sasa timu hiyo inanolewa na mmoja wa makocha bora kwa soka la Afrika, Otto Pfister kutoka Ujerumani.

Sasa ni juu ya vijana wetu kupata mabao mengi hapa nyumbani kama tulivyofanya katika mchezo wetu dhidi ya Petro du Luanda ambapo tulishinda 3-0 nyumbani. Tatizo kubwa tuliloliona katika timu yetu ni umaliziaji. Kocha wetu Micho inabidi ajitahidi kuimarisha fowadi yetu ndani ya wiki 2.

Kwa upande wao viongozi inabidi waache wachezaji wacheze mpira na si kutoa kauli kwamba tutashinda 5-0 bila kufahamu hali halisi ya timu yako.


Nawatakia maandalizi mema wachezaji wetu katika kukabiliana na vigogo hao wa Sudan hapo terehe 5 Mei 2007 katika mechi ya kwanza hapa nchini.

MUNGU IBARIKI YANGA NA TANZANIA

6 comments:

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe kabisa CM. Maandalizi ya nguvu na mapema ni muhimu. Tunahitaji kuwafunga hawa jamaa mabao mengi tuu. Sii chini ya matatu, ili kujiweka ktk mazingira mazuri.

Mungu Ibariki Yanga na Tanzania.

Anonymous said...

Kwatuliokuwepo Mwanza na mazungumzo tuliyofanya pale La Cairo Hotel baada ya mechi nafikiri ni muda muafaka Micho asikumbatie majina ya wachezaji UMALIZIAJI UMEKAA VIBAYA jamani ni vema asiachiwe peke yake upangaji wa timu akubali ushauri. SUDAN NI WETU .

Anonymous said...

kwa mimi nigeshauri kipindi cha kwanza wasimchezeshe MWAIKIMBA bali wamtangulize NGASA kwani wenyewe huwa mnaona jinsi NGASA anavyo badilisha mchezo akiingia na sio huyo MWAIKIMBA.
by Mkereketwa nambari 1

Anonymous said...

Wadau mmeonaje kocha akianza kujenga combination ya Gula na Mourice halafu pembeni awatupe SMG na Ngassa?

Mikundu Matako Makalio Manundu said...

Tunawaombea Yanga watutowe kimaso-maso, tuna kila sababu za kuwashinda Merekh, kwanza wa-Sudani tunawajuwa tushacheza nao sana tuu, pili ni mkufa na kupona.

Nimefurahi kuikuta blogu hii...uiendeleze na sisi tutakupa tafu.

Halafu msisahau kupitia Kwa Mzee wa Mi...du, leo kuna Mambo ya Brazili, kesho sijui nini kitakuwepo:
http://mikundu.blogspot.com/

http://mikundu.blogspot.com/

http://mikundu.blogspot.com/

Anonymous said...

Nadhani combination ya Gula na Moris, kisha SMG na Ngasa pembeni, pamoja na Abdi Kassim inaweza kuzaa mtunda mazuri. Ila pia nashauri kazi ya ziada ifanyike washambuliaji wa-shuti golini. Hilo sijui ni washambuliaji wenyewe ama kocha, maana sielewi inakuwaje mchezaji anapewa pasi yeye na kipa halafu ama unazubaa hadi mpira unaokolewa au unatoa tena pasi?

Kumpa ushauri kocha ktk upangaji wa timu nadhani ni sawa, ila uamuzi wa mwisho uwe wake. Yeye ndo yuko responsible timu ikifanya vibaya, sio wale walompa ushauri. Pia yeye anakuwa na wachezaji kwa muda mwingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, kwa hiyo anakuwa anajua their state physically and psychologically.