Tuesday, May 15, 2007

Fomu za Uongozi hizo! Jitokezeni sasa

Ofisi ya Msajili Msaidizi wa Vyama na Klabu Wilaya ya Ilala, jana ilianza kutoa fomu za kuwania uongozi wa Klabu ya Yanga hapo Mei 26.

Sasa ni juu ya wanachama wenye nia na sifa za kuwania uongozi kujitokeza kwani mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Mei 18.


Akizungumza katika ofisi hizo jana, Msajili Msaidizi wa Vyama na Klabu za michezo Wilaya ya Ilala, Penina Maduhu, alisema aliyechukua jana ni Hamis Kinye anayewania kuwa Katibu Mwenezi.

Aidha, kamati ya kuhakiki kadi za wanachama, imesema ya kuwa, zoezi la uhakiki lilikuwa lifungwe jana, lakini sasa litafungwa leo ili kuwapatia nafasi wale walioshindwa kufanya hivyo katika muda uliopangwa awali.

Hadi jana wanachama waliokuwa wamehakikiwa walikuwa ni 735. Yanga imeamua kuhakiki wanachama wake ili kujua ina wanachama hai wangapi watakaoshiriki kwenye uchaguzi na pia kununuliwa hisa moja kila mmoja wakati klabu hiyo itakapoanza kuuza hisa zake.

Mapema mwaka huu, mfadhili wa timu hiyo Yusuf Manji alitangaza nia yake ya kuwanunulia hisa wanachama wa klabu hiyo pindi klabu hiyo itakapouza hisa za Kampuni ya Young Africans Sports Corporation Limited. Ununuzi huo wa hisa ni moja ya utekelezaji wa waraka wa muafaka wa klabu hiyo.


1 comment:

Anonymous said...

Haya, wale wenye nia njema ya kuendeleza klabu yetu wajitokeze. Nia iwe ni kuifanyia klabu kitu, sio klabu ikufanyie wewe.

Tunahitaji viongozi wenye vision. Ambao wataepuka migogoro isiyo ya lazima na kuiendesha klabu ki-taasisi.

Kila la kheri uchaguzi Yanga.