Monday, May 14, 2007

Safarini Sudan kupitia Ethiopia

Kikosi cha wachezaji 19 wa Yanga kiliondoka nchini jana kuelekea Ethiopia kujiandaa na pambano lake la marudiano dhidi ya El Merreikh ya Sudan litakalofanyika mwishoni mwa wiki katika mchezo wa marudiano wa raundi ya 4 ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wachezaji walioondoka jana kuwa ni Ivo Mapunda, Jackson Chove, Shadrack Nsajigwa, Abuu Mtiro, Wisdom Ndlovu, Nadir Haroub `Canavaro', Hamis Yussuf, Edwin Mukenya, James Chilapondwa na Mrisho Ngassa.

Wengine walioondoka jana ni Credo Mwaipopo, Waziri Mahadhi, Amri Kiemba, Abdu Kassim, Hussein Sued, Abuu Ramadhani, Said Maulid `SMG`, Amir Maftah na Thomas Maurice. Mshambuliaji Gaudence Mwaikimba ataondoka leo baada ya hati yake ya kusafiria kuwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Yanga Francis Kifukwe ambaye alirejea jana kutoka safarini Nairobi, Kenya.

Timu hiyo itaongozwa na kocha wa makipa Razak Siwa. Kocha wa timu hiyo Milutin Sredovejic 'Micho' tayari ametangulia huko Ethiopia ambapo timu hiyo itaweka kambi kwa siku tatu.

Yanga inahitaji sare ya magoli au ushidi ili iweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

No comments: