Thursday, May 10, 2007

Uhakiki wa wanachama kuanza kesho

Mchakato wa uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga unatarajiwa kuanza kesho kwa uhakiki wa wanachama wa Yanga waliopo mkoa wa Dar es Salaam.

Akitangaza utaratibu huo, mmoja wa viongozi wa zoezi la uchaguzi wa Yanga Bw. Lucas Kisasa amesema zoezi hilo la kuhakiki wanachama ni mwanzo wa kuelekea kwenye uchaguzi utakaofanyika Mei 26. Zoezi la kuhakiki wanachama hao linatarajiwa kumalizika Jumatatu ijayo. Utaratibu wa kuhakiki wanachama waliopo mikoani linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Yanga kwa sasa inaongozwa na kamati ya mpito inayoongozwa na Francis Kifukwe akisaidiwa na Mzee Yusuf Mzimba. Uongozi wa awali wa Yanga ulimaliza muda wake Machi mwaka huu, ukiwa chini ya Rais Francis Kifukwe.

Sare na Polisi Moro
Wakati huo huo Yanga imetoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya ligi ndogo ya TFF kituo cha Arusha.

Yanga ilitangulia kufungwa mapema katika kipindi cha kwanza lakini ilisawazisha katika dakika za mwisho kupitia kwa Hussein Swedi.


Yanga imemaliza mechi zake katika kituo hicho ikiongoza kwa kujikusanyia pointi 12.


No comments: