Wednesday, May 09, 2007

Yanga yatoa 6 Taifa Stars

Kocha wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo, ametangaza kikosi kipya cha timu hiyo huku Yanga ikitoa wachezaji 6.

Mshambuliaji ambaye amekuwa akilalamikiwa sana hasa na wana Simba, Gaudence Mwaikimba ameachwa katika kikosi hicho. Mchezaji mwingine wa Yanga ambaye hajaitwa katika kikosi hicho ni Yusuf Hamis.

Wachezaji waliobahatika kupata nafasi ya kuwemo Taifa Stars ni:

Makipa:
Ivo Mapunda (Yanga), Ally Mustapha (Simba), Soud Slim (Mtibwa)

Mabeki wa Pembeni:

Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Vital'O), Mecky Mexime (Mtibwa), Ibrahim Mwaipopo (Mtibwa), Yasin Juma (Pangolin Academy).

Mabeki wa kati:
Abdulahim Amour (Ashanti), Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga), Salvatory Ntebe (Vital'O), Salum Sued (Mtibwa), Victor Costa (Simba).

Viungo:
Abdi Kassim (Yanga), Amir Maftah (Yanga)
, Haruna Moshi (Simba), Henry Joseph (Simba), Juma Said (Ashanti), Kigi Makasi (Makongo), Maregesi Mwangwa (Kagera Sugar), Nizar Khalfan na Shaaban Nditi (Mtibwa).

Washambuliaji:
Danny Mrwanda (Simba), Said Maulid (Yanga), Jerry Tegete (Makongo), Joseph Kaniki (Simba) na Vicent Barnabas (Kagera).

Taifa Stars inajiandaa na mechi mbili za kufuzu kuingia kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika huko Ghana mwakani. Taifa Stars itapambana na Senegal Juni 2 huko Mwanza kabla ya kuifuata Burkina Faso wiki mbili baada ya hapo.

Wakati huo huo leo Yanga inaingia uwanjani kupambana na Polisi ya Morogoro katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya ligi ndogo kituo cha Arusha, mchezo utakaofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

3 comments:

Anonymous said...

Siiombei mabaya Stars, lakini nadhani Maximo tayari ameanza kulewa na siasa za mpira wa tanzania. Alichofanya ni kuchagua wachezaji 6 toka simba ya yanga (just balancing the numbers) na kuchukua wachezaji wengi wa mtibwa ili simba na yanga zisiwe na majority number. Hizo ndo siasa.

Wachezaji kama Hamis Yusuf, Athuman Idd na Mrisho Ngassa (sijui kwa nini hajamwita huyu dogo) wangestahili kuwepo.
Naamini uzoefu wa mechi za kimataifa ni muhimu.

Hao wengine wangeitwa baada ya mechi ya senego wakafanya mazoezi kwanza na kucheza mechi za kimataifa.

Sitashangaa senego wakitupiga goli 5 kirumba... naomba siku hiyo apangwe kipa wa simba.... (jocking..)

Mwaikimba acha apumzike kidogo, Simba nao wachezeshe strickers wao tuone... (utadhani hawakuwepo wakati wanatolewa na kitimu cha msumbiji)

Anonymous said...

Huyu anonymous wa hapo juu mbona hajui anachoongea ? Mambo ya mpira wa miguu atuachie siye na yeye aendelee na mambo ya netiboli !!!!

lititu said...

ila tuacheni utani forward yetu inapwaya vibaya mno yaani ufungaji ni sifuri