Tuesday, May 08, 2007

Kununua mechi imekuwa noma?

Wanachama watatu wa Klabu ya Yanga wamevuliwa uanachama wao na Kamati ya Muda ya klabu hiyo baada ya kuthumiwa kuuhujumu muafaka na hali ya amani iliyopo klabuni hapo.

Katika taarifa iliyotolewa na Uongozi wa muda wa Klabu hiyo, imewataja wanachama hao kuwa ni Kibo Merinyo, Juma Magoma na A. Mwaipopo.

Pia klabu hiyo ilimtaka Kibo Merinyo apeleke taarifa ya fedha ya mechi 2 za Yanga dhidi ya Petro du Luanda pamoja na ile ya Esperance.

Akina Merinyo walihoji matumizi ya fedha za mechi zilizotolewa na mfadhili wa Yanga Bw. Yusuf Manji ambaye alinunua mechi hiyo kwa shillingi millioni 100. Wanachama hao walikuwa wakitaka kujua fedha hizo zimeingia kwenye akaunti gani.

Naye Merinyo amedai kwamba hawezi kufukuzwa kwa vile waliomfukuza sio wanachama wa kuchaguliwa.

Hivi karibuni wanachama kadhaa wa klabu hiyo walikwenda kwenye ofisi ya gazeti moja Jijini, kutoa malalamiko yao dhidi ya mfadhili wa timu hiyo - Manji wakimtuhumu kwamba anaikopesha Yanga badala ya kuifadhili.

Moto ndiyo huo umeanza kichini chini, tuombe Mungu hizi hela za Manji zisitugombanishe.


Mungu Ibariki Yanga.

4 comments:

Anonymous said...

Sasa huu ni upeezi wewe tayari umekuwa mdomo wa akina Merinyo, mimi nilifikiri hii site ni haifungamani na upande wowote?
Ipo kazi

CM said...

Habari nilizotoa ni kwamba wanachama 3 wamefukuzwa na mmoja wa hao wanachama amepinga kufukuzwa. Sasa hapo nimeegemea upande gani?

Sijaona kama nimetetea kundi lolote. Hata hivyo Yanga ni moja kwa sasa. Sasa mtu anapohoji suala la kuegemea upande mmoja naomba afafanue hizo pande zilizopo Yanga ni zipi?

Hebu naombeni maoni zaidi wadau. Labda mmenielewa tofauti.

Shukrani.

Anonymous said...

CM Umeeleweka vizuri tuu. Wala hujaegemea upande wowote. Huyo bwana labda hakukuelewa.

Mimi jamani tatizo langu ni hawa wanaojifanya wanachama na wana uchungu na klabu kumbe janja tuu ya kuiba hela za viingilio.

Niliwaona kwenye gazeti (picha) na makanzu yao, eti wanauliza kwa nini mechi iuzwe, kumbe walitaka wakae milangoni, baadaye waseme zimepatikana sh. million 50 badala ya million 100. Hamsini wanatia ndani.

Mimi nadhani wakati umefika wa kuacha kuendekeza njaa kwenye vilabu vyetu. hawa kina Merinho (Merinyo) ndo wanaoibua migogoro kila siku ili waendelee kunufaika binafsi, huku wachezaji wakiishi maisha ya tabu.

Mimi na-suggest mechi zote ziuzwe. Iwekwe kampuni ya kukusanya mapato at a fee.

Huwa inashagaza inaambiwa mechi wa Simba na Yanga imeingiza watu 20,000 tu, wakati uwanja wa taifa ulijaa tii.. kumbe hao wanaojiita makomamdoo wanakuwa wameweka mifukoni hela za watu wengine kama 20,000 hivi.

Recently, nilihudhuria mechi zote za Yanga za ligi ndogo hapa Arusha, na several times unaenda kununua ticket unaambiwa zimeisha, unalipa hela na kuingia bila ticket. Nadhani hela zote hizo zinaingia mifukoni kwa kina merinho... wadau mnaonaje?

Anonymous said...

Watu wanageuza Yanga kuwa ni sehemu ya kuendeshea maisha yao. Tatizo ni kwamba ukiweka system ya kuwabana hawa makomandoo, utasikia mgogoro mkubwa unafumuka klabuni.

Mtani wetu Kaduguda aliwahi kusema Simba na Yanga ni Viwanda. Watu wanaendesha biashara zao, wanapendeza mjini kupitia vilabu hivi.

Wanaoleta chokochoko klabuni ni watu wa kufukuzwa tu. Njaa ndiyo inawasumbua.