Thursday, May 31, 2007

Madega kuongoza Yanga

Imani Omar Madega - Mwenyekiti wa Yanga

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Pwani (COREFA) na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF, Imani Omar Madega amefanikiwa kutwaa Uenyekiti wa klabu ya Yanga katika uchaguzi wa Klabu hiyo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Madega alikuwa akipambana vikali na mgombea mwingine Mbaraka Igangula, wamepata kura 715 na 238 kwa kufuatana (respectively).

Nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti imekwenda kwa Rashid Ngozoma Matunda aliyepata kura 875 akimshinda Shaban Dilunga (56). Patrick Fata alijitoa kugombea nafasi hiyo.

Nafasi nyeti ya Ukatibu Mkuu ilikwenda kwa Lucas Kisasa aliyepata kura 689 akiwashinda Costantino Maligo (147) na Emmanuel Mpangala (88).

Nafasi nyingine
Katibu Mkuu Msaidizi: Ahmed Mamba
Mweka Hazina: Abeid Mohamed Abeid 'Falcon'
Mweka Hazina Msaidizi: Godfrey Mwanje
Katibu Mipango: Patrick Fata
Katibu Mwenezi: Francis Lucas

Tunawatakia kila la heri viongozi wetu wapya. Yanga Imara Daima mbele.


3 comments:

Anonymous said...

WANDUGU HABARI NILIZOZIPZTA HIVI KARIBUNI NI KWAMBA KIPA WA ZAMANI WA YANGA BERNARD MADALE AMEFARIKI DUNIA JANA 6/6/2007. MUNGU AMUWEKE MAHALI PEMA PEPONI . AMINA.

Anonymous said...

RIP

Kwa faida ya Wana Yanga wengi tulioanza kuifahamu Yanga ndani ya miaka 20 iliyopita, hebu tukumbushe marehemu alikuwa kwenye kikosi cha mwaka gani?

Nanuri Safari said...

BEN MADALE kipa aliyefungwa 6 Bila na Simba. RIP