Tuesday, May 29, 2007

Uchaguzi sasa Diamond Jubilee

Wakati baadhi wa wanachama wakilalamikia kufanyika kwa uchaguzi katikati ya wiki, Ukumbi kwa ajili ya uchaguzi umebadilishwa kutoka Karimjee na sasa utafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Baadhi ya wanachama wa Yanga wanataka uchaguzi huo kusogezwa mbele kwa sababu kesho ni siku ya kazi, hivyo kuwawia vigumu kushiriki kikamilifu katika shughuli hiyo.


Hata hivyo kama utasogezwa hadi mwishoni mwa wiki hii uchaguzi huo pia unaweza kuathirika kwa vile kuna mechi kubwa ya Kimataifa kati ya Taifa Stars na Senegal ambayo itafanyika Mwanza na huenda wanachama wengi wakaeleka huko.

Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Jumamosi iliyopita lakini uliahirishwa hadi kesho kufuatia
orodha ya wanachama iliyo kwa Msajili kutofanana na marekebisho ya katiba ya mwaka 2007 na pia karatasi za kura zisingeweza kuchapishwa kwa siku moja kufuatia zoezi la usaili kuchelewa kumalizika.


Wakati huo huo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi Ally Bwamkuu amejito a katika kinyang'anyiro hicho.

Bwamkuu amejitoa kwa madai kwamba tayari matokeo yameshapangwa na hivyo kushiriki kwake ni kazi bure tu.

No comments: