Monday, May 28, 2007

Wagombea wetu

Mwenyekiti:
Ismail Idrissa, Imani Madega, Rashid Bhinda, Kibo Merinyo na Baraka Igangula

Makamu wa Mwenyekiti:
Rashid Ngozoma Matunda, Shabaan Dilunga na PatrickFata.

Katibu Mkuu:
Lucas Kisasa, Constantine Maligo na Emmanuel Mpangala.

Katibu Msaidizi:
Ahmed Mamba, Mlimuka Luhanda, Ally Bwamkuu, Francis Kaswahili, Said Motisha, Abdulrahman Gwando, Constantine Maligo, Mohamed Bhinda, Rasul Ndee na Ramesh Patwa.

Katibu Mipango:
Ismail Mwapani, Seif Mohamed, Yussuf Yassin, Ali Kamtande, Geoffrey Mhagama na Patrick Fata.

Katibu Mwenezi:
Hamisi Juma, Francis Lucas, Bakili Makele, Juma Magoma, Mlimuka Luhanda, Bakari Malima, Hamisi Kinye, Mohamed Omar na Makusudi Hussein.

Mweka Hazina:
Patory Kyombya, Abeid Mohamed Abeid, Castory Nketto na Jeremiah Mkali.

Mweka Hazina Msaidizi:
Abbas Bomba, Boniphace Clemence, Godfrey Mwenge na Seif Mbelwa.

UCHAGUZI UTAFANYIKA JUMATANO TAREHE 30/05/2007 KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE.

Kama kuna mwanablog yeyote anayefahamu sifa za hawa wagombea ni vizuri atuwekee wazi bila majungu ili tujue nani ni nani.

Nawasilisha.


5 comments:

Anonymous said...

Nasikia kuna wanachama kibao wa Yanga wenye kadi za miaka ya 1960 ambao hawakujitokeza kuhakikiwa ili wafanye uchaguzi lakini waliposikia mshiko wa sh. 20,000/- wakajitokeza kuchukua?

Kama ni kweli basi nadhani viongozi wapya wana kazi kubwa ya kufanya. Maana wanachama wanatakiwa kwenda klabuni kutimiza wajibu na haki yao ya kupiga kura hata kama hawaahidiwa kulipwa kitu. Sasa kumbe wako wengi na kadi wanazo lakini hawajitokezi?

Jamani wanachama tunatakiwa kupeleka hela klabuni, sio kwenda kuchukua hela... Hii elimu mpaka ituingie akilini itachukua muda.

Anonymous said...

Ingekuwa vizuri wagombea wenyewe wakapitia hapa na kuweka sera zao hadharani. Lakini huenda wapenzi wengi wa hapa nyumbani hawaijui hii blog 'yetu'.

Kuna gazeti pale klabuni nadhani linaitwa 'Sauti ya Jangwani' kama sijakosea. Sasa kama unaweza pata email ya mhariri unaweza kumpa details za hii blog akachapisha kwenye hilo gazeti, ili viongozi na wanachama nao wawe wanatembelea hapa, nakutoa maoni yao.

JM.

Anonymous said...

Hapa kuna maelezo kidogo ya baadhi ya Wagombea. Ni kutoka gazeti la Tanzania Daima la leo:

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/28/makala2.php

Sina hakika kama hakuwa akipigiwa debe mtu, lakini its worth reading (inafaa kusoma..).

JM.

CM said...

JM nakushukuru sana kwa michango yako mbalimbali ambayo kusema kweli huwa inanijenga sana.

Nimejaribu kutafuta hilo gazeti la Sauti ya Jangwani nimeona wametoa mawasiliano yao na nimefanikiwa kupata email yao (jangwani2007@yahoo.com) kwa hiyo kama mdau yeyote atafanya mawasiliano nao au vinginevyo asisite kudondosha data hapa bloguni

Kuhusu hiyo makala iliyopo kwenye TZ Daima naona kama wanapiga kampeni sehemu fulani.

Kichwabuta Mwendantwala said...

Huyo Patrick Fata, anayegombea Umakamu Mwenyekiti na Ukatibu Mipango mbona naambiwa ya kuwa HANA kabisa uzoefu na hizo nafasi anazogombea kwani hata wafanyakazi wenziwe wa Benki Kuu ya Tanzania wanasema hajawahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote pale ofisini kwake !!! Sasa tukimpa hizo nafasi anatuahakikishaje kama ATAZIMUDU ?????