Wednesday, May 23, 2007

Wengi wachangamkia fomu Yanga

Hekaheka za kuelekea kwenye uchaguzi zinaendelea Jangwani ambapo leo ndiyo siku ya mwisho ya wanachama wa klabu hiyo kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo.

Hadi sasa baadhi ya wanachama waliochukua fomu na nafasi zao ni kama inavyoonyeshwa hapo chini:

Mwenyekiti
Rashid Bhinda, Kibo Merinyo, Iman Madega, Ismail Idrissa

Makamu Mwenyekiti
Shaban Dilunga. Abdulrahman Bwando

Katibu Mkuu:
Costantine Maligo na Lucas Kisasa.

Katibu Msaidizi :
Said Motisha, Ahmada Mamba, Mwinuka Luhanga, Ally Bwamkuu, Israel Mwapwani, Francis Kaswahili na Abdulrahman Bwando.

Katibu Mipango
Yusuph Yassin, Emmanuel Mwakila, Bakili Makere, Harun Kasonso na Ally Mussa Kamtande.

Katibu Mwenezi
Mwinuka Luhanga, Hamis Kinye, Emmanuel Mwakila, Mohamed Othman, Mohamed Bhinda, Bakili Makere, Hussein Makusudi, Francis Lucas na Bakari Malima.

Mweka Hazina
Boniface Clemence, Abeid Mohamed na Pastory Kyombya.

Mweka Hazina Msaidizi
Boniface Clemence, Felix Nyanza, Godfrey Mwenje.

Fomu zinaendelea kutolewa leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu hizo. Usaili wa wagombea utafanyika kesho katika ukumbi wa Karimjee na uchaguzi umepangwa kufanyika Jumamosi katika Ukumbi huohuo.

Wanachama wenye nia kugombea leo ndiyo siku ya mwisho kwenu kuchukua fomu. Kazi kwenu.

1 comment:

Anonymous said...

Nilipata kuuliza kama inawezekana wagombea wetu wakatoa maelezo yao binafsi kwenye magazeti ama hapa kwenye blog, maana sijui kama wanachama wanajua nini hao wagombea wanataka kuifanyia klabu !.

Pia sijui kama kuna mtu anajua sifa (qualifications) za mtu kama Mweka Hazina na Msaidizi wake. Nadhani kwa klabu kubwa kama Yanga hawa watu wanatakiwa kuwa na minimum CPA au degree ya pili ktk finance, uchumi, MBA, etc. Maana kazi hasa sio 'kuweka-hazina', bali 'kutafuta na kutunza' hazina za klabu. Utafutaji unahitaji elimu.

Lakini kwa sasa maswali mengi hayasaidii. Tuombe tuu uchaguzi ufanyike na wapatikane viongozi wapenda maendeleo, kisha hawa wasimamie full overhaul ya katiba ya Yanga iweze kwenda na hali ya sasa ya soka la dunia.

Kila la kheri wagombea na wanachama. Ila sasa na wale watakaoshindwa wakubali matokeo na kushirikiana na watakaoshinda, sio kuanzisha tena makundi na migogoro.

JM.