Friday, June 08, 2007

Kampuni au Klabu?

Kuna utata wa kikatiba umegubika miongoni mwa wana Yanga baada ya wengi kuwa na wasiwasi kwamba uongozi uliochaguliwa hivi karibuni watalazimika kuwajibika chini ya uongozi wa Kampuni mpya ya Young Africans Sports Club Corporation.

Hata hivyo uongozi mpya uliochaguliwa umedai kwamba wao ndiyo wanaoongoza klabu ambayo itakuwa inamiliki 51% ya hisa za kampuni hiyo. Imebainishwa kwamba Kampuni hiyo itakuwa inajishughulisha zaidi na masuala ya biashara wakati mambo ya wachezaji yatakuwa chini ya uongozi mpya wa klabu ulioingia madarakani hivi karibuni.

  • Maswali ambayo baadhi ya wana-Yanga wanajiuliza ni kwamba kama Uongozi wa Kampuni utakuwa chini ya Rais, sasa kati ya Rais na Mwenyekiti ni nani mwenye nguvu zaidi?
  • Masuala ya fedha za klabu na yale ya Kampuni yatasimamiwa na Mweka Hazina aliyechaguliwa au itabidi Yanga itangaze ajira kwa nafasi zote za Uongozi katika Kampuni ili uwajibikaji uongezeke?
Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kuwekwa wazi na kama kuna mdau ana ufahamu wa katiba ya klabu yetu atudondoshee hapa bloguni. Nia ni kueleweshana na si kuchimba amani iliyopo klabuni.

Naomba kutoa hoja.




1 comment:

Anonymous said...

Personally sina details zilizoko ktk marekebiso ya katiba mpya, ila nadhani kutakuwa na mgawanyo mzuri wa madaraka kati ya klabu na kampuni.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kabla ya uchaguzi nilielewa kwamba klabu itamiliki 51% ya hisa za kampuni. Kampuni itaendeshwa na Raisi, bila shaka atachaguliwa na wanahisa, na viongozi wengine. Wafanyakazi wengine wa Kampuni bila shaka wataajiriwa on merits.

Pia ilisemwa kuwa Kampuni itakuwa na jukumu la kuhudumia timu (hapa nadhani ni zaidi financially), yaani kulipa mishahara ya wachezaji na makocha, kuhudumia kambi, kununua vifaa vya michezo, kuingia mikataba na wadhamini, nk.

Kwa maana hii, kweli kampuni itakuwa na sauti kubwa ktk timu, lakini tusisahau kuwa Klabu ndio major shareholder kwenye kampuni.

Naamini viongozi wapya wanafahamu vizuri muundo huu mpya wa klabu na kampuni. Na labda mwanachama/mdau mwenye details zaidi anaweza kutupa mwanga zaidi hapa bloguni.

JM.