Wednesday, June 27, 2007

Leo tunajiuliza kwa JKT Ruvu

Ligi ndogo ya TFF hatua ya sita bora inaendelea tena kwa Yanga kupambana na JKT Ruvu katika mchezo wa kundi A utakaochezwa huko kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Timu hizo mbili zinachagizwa na ushindi waliopata dhidi ya Mtibwa Sugar hivi karibuni. Yanga iliifunga Mtibwa Sugar 3-2 wakati JKT Ruvu ilishinda 3-1.

Mchezo huo unatarajia kuwa mgumu kwani Yanga huwa inapata taabu sana kuifunga JKT Ruvu inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Yanga, Fred Felix Minziro.

Mpaka hapo baadaye, kila la heri Yanga.


5 comments:

Kichwabuta Mwendantwala said...

Nawatakia kila la kheri timu yetu ya YANGA ili iweze kufanya vizuri leo dhidi ya vijana wetu wadogo wa JKT Ruvu. Na sina shaka tutatoka KIFUA MBELE kwa bao 2 - 1, na huo ndio utabiri wangu. Mungu wabariki wachezaji wa YANGA, Mungu ibariki YANGA !!!!

KICHWABUTA MWENDANTWALA said...

TUNAOMBA MATOKEO KATI YETU NA RUVU JKT (YA LEO) HARAKA KWANI TUNA HAMU NAYO SANA !!!!

Anonymous said...

0-0

Kichwabutwa Mwendantwala said...

"Tunaomba uwepo utaratibu wa kuwa mnatupa matokeo hata wakati mpira ukiwa bado unaendelea kwani huwa tunakuwa na wasiwasi na timu yetu inapocheza ................ "

JZah said...

Ndugu yangu Kichwabutwa, nadhani unaelewa kuwa hilo ombi lako ni investment kubwa kwa CM. Ku-update blog wakati mpira unaendelea ina maana inabidi awepo uwanjani akiwa na laptop iliyokuwa connected kwenye internet, kila timu inapocheza. Sio kwamba hilo haliwezekani ila i think it is too much to ask of CM! Ukizingatia gharama za maisha na technology kwa bongo, ni vigumu ku-sustain ombi lako hata kama angependa kufanya hivyo.

Wewe na mimi na wengine tunaweza kuiwezesha Yanga kuwa na website yake ambayo itakuwa updated kila timu inapocheza. Hizi timu zinapaswa kuweka record zake electronically. Mfano ukiuliza leo Said Maulid amefunga magoli mangapi tangu amejiunga Yanga au Ivo Mapunda amecheza mechi ngapi Yanga hakuna mtu atakupa record. Lakini system ikiwa developed kushirikiana na viongozi wa klab hili linawezekana. Wenzetu wanafanya hivyo. Makocha kama Micho najua wanaweka record hizi zote, to the details za mchezaji fulani amepiga cross ngapi au attempts ngapi to the goal. Lakini wakiondoka wanaondoka na tarifa zao, sababu hatuna utaratibu wa kuziweka.

Na sisi kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake, mambo mengi yanaweza kufanyika.

JM aka JZah