Thursday, June 28, 2007

Yanga vs JKT Ruvu: 0-0

Yanga jana ilishindwa kutwaa uongozi wa ligi ndogo hatua ya 6 bora kituo cha Arusha baada ya kutoka sare ya 0-0 na JKT Ruvu katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

JKT Ruvu na Yanga zote zina pointi 4 lakini JKT Ruvu inaizidi Yanga kwa tofauti ya goli moja. Timu hizo mbili zilijipatia ushindi katika mechi zake za kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar. Yanga ilishinda 3-2 wakati JKT Ruvu ilishinda 3-1.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa kwa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar.

No comments: