Saturday, June 30, 2007

Yanga na Mtibwa kurudiana leo

Mzunguko wa pili wa ligi ndogo ya TFF hatua ya sita bora inaendelea leo na katika kituo cha Arusha, Yanga itakumbana na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu sana hasa ukizingatia kwamba hadi sasa Mtibwa haina pointi hata moja baada ya kupoteza michezo yake miwili ya awali na itataka kuweka hai matumaini yake ya kuwania ubingwa. Yanga nayo itataka kuweka hai matumaini yake ya kutwaa uongozi wa kundi hilo.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilishinda 3-2.

Kwa hiyo mdau yeyote atakayepata matokeo mapema anaweza kudondosha mambo hapa kwenye comments. Kila la heri Yanga.

4 comments:

Anonymous said...

Hadi sasa ni Halftime. Tunaongoza 1-0 mfungaji akiwa ni Amri Kiemba(35) - CM

Anonymous said...

Matokeo hadi mwisho:
Yanga 2 - 1 Mtibwa

Goli letu la pili limefungwa na Tomas Morris (dk. 90)

Hapa naona mambo yameiva.. kilichobaki ni kumfunga JKT mechi ijayo na kwenda final with Simba.

JM.

Anonymous said...

Tumeshinda 2-1. Goli letu la ushindi limepatikana dk ya 90 kupitia kwa Thomas Mourice. Sasa tuna pt 7.
CM

lusekelo hudson said...

Du nimefurahi sana vijana wanastahili pongezi lusekelo Santiago De Cuba