Monday, July 02, 2007

Yanga kusikilizia Mtibwa na JKT Ruvu

Hatma ya njia ya Yanga kumaliza mshindi katika kituo cha Arusha itajulikana leo kwa timu za JKT Ruvu na Mtibwa Sugar kuumana katika mchezo wa kundi A utakaofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

Endapo JKT Ruvu itashinda mchezo huo kwa mabao mengi, basi timu hiyo itahitaji sare tu dhidi ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Yanga keshokutwa. Hali inazidi kuwa ya wasiwasi kwa Yanga hasa ukizingatia kuwa Mtibwa haina nafasi ya kuchukua ubingwa, kwani hata ikishinda itakuwa imejikusanyia pointi 3 ambazo tayari zimevukwa na Yanga na JKT.

Kwa muda leo inabidi tuwe mashabiki wa Mtibwa Sugar ili icheze kwa kulinda heshima ya kumaliza ligi angalau na pointi kibindoni.

- Shukrani kwa wadau kwa kutoa matokeo ya mechi iliyopita mapema.
Kwa wale ambao hawajapata matokeo, Yanga ilishinda 2-1

2 comments:

Anonymous said...

JKT Ruvu imepata kichapo cha 2-3. Sasa tunahitaji sare tu ili tucheze michuano ya Afrika mwakani. - CM

Anonymous said...

Shukrani kwa kutoa matokeo mapema.

Naomba vijana wasiwadharau hao JKT ingawa wanafungika. Lengo liwe kuwapiga bao nyingi tuu, na sio sare. Nina hamu ya kukutana na Simba kwenye final.

Lina la kheri chama langu.