Tuesday, July 03, 2007

Mtibwa warahisisha njia lakini........

Timu ya Mtibwa Sugar jana iliiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutwaa ushindi wa kwanza katika kituo cha Arusha baada ya kuifunga JKT Ruvu 3-2 katika mchezo wa kundi A wa ligi ndogo ya TFF kituo cha Arusha.

Kwa ushindi huo sasa Yanga inahitaji sare tu ili kuwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa mwakani. Yanga ina pointi 7 wakati JKT Ruvu imebakiwa na pointi 4.

Wakati hali ikiwa nzuri kwa upande wa matokeo hayo, balaa kubwa limewakumba wachezaji 15 wa Yanga pamoja na kocha Micho baada ya wachezaji hao kula chakula ambacho kinasemekana kuwa na sumu, hali inayowasababishia madhara ya tumbo.

Wachezaji hao ambao walikuwa wakitapika na kuharisha mara kwa mara, walidhurika baada ya kula samaki juzi usiku.

Hali hii ya wachezaji inaiweka Yanga katika wakati mgumu hasa ukizingatia kwamba kesho wanacheza na JKT Ruvu ambayo inatafuta ushindi ili iipiku Yanga katika kilele cha msimamo wa kundi A.

Tuwaombee wachezaji wetu uzima ili tusije tukakosa hata hiyo pointi moja tunayotafuta.

No comments: