Wednesday, July 04, 2007

Tutaingia fainali leo?

Yanga leo inatupa karata yake ya mwisho katika mchezo wa ligi ndogo ya TFF hatua ya sita bora kwa kuchuana na JKT Ruvu katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha.

Yanga inaingia katika mchezo huo huku ikihitaji sare tu huku wapinzani wao JKT wanahitaji ushindi ili iweze kuiengua Yanga na kuingia fainali ya michuano hiyo dhidi ya mshindi wa kundi B ambalo linacheza mechi zake huko Morogoro.

Siku mbili zilizopita afya ya wachezaji wa Yanga haikuwa katika hali nzuri kufuatia wachezaji wengi kushikwa na ugonjwa wa tumbo likiambatana na kutapika baada ya chakula walichokula kusemekana kuwa na sumu. Hata hivyo hali ya wachezaji hao imetengemaa tayari kwa pambano hilo la leo.

Tunawatakia afya njema na mchezo mwema wachezaji wetu.

3 comments:

Anonymous said...

Tumefanikiwa kutoka sare 1-1 na JKT, hivyo tutacheza fainali na Simba ambayo imefanikiwa kushinda ktk kituo cha Moro.

Mengi zaidi kesho.

CM

Anonymous said...

asante sana cm kwa matokeo ya haraka maana wengine tulikuwa twasubiri update kwa hamu

Son of a peasant

Kichwabuta Mwendantwala said...

Tunaombeni mikakati ya jinsi ya KUIFUNGA SIMBA SAFARI hii maanake tumechoka kufungwa na hawa watani wetu kila kukicha !!!