Thursday, July 05, 2007

Ni fainali ya kufa mtu

Wakongwe wa soka nchini Yanga na Simba, watachuana Jumapili katika mchezo wa fainali ya kutafuta mshindi wa ligi ndogo ya TFF baada ya timu hizo mbili kuibuka washindi katika vituo vya ligi hiyo ndogo hatua ya sita bora.

Yanga imeibuka mshindi katika kituo cha Arusha baada ya kutoka sare ya 1-1 na JKT Ruvu na kufanikiwa kujikusanyia pointi 8 ikifuatiwa na JKT Ruvu waliomaliza na pointi 5. Mtibwa Sugar iliambulia pointi 3.

Katika kituo cha Morogoro, Simba iliibuka mshindi wa kituo hicho baada ya kuitandika Polisi Moro kwa mabao 3-0. Simba imemaliza ikiwa na pointi 10 ikifuatiwa na Polisi Moro iliyojikusanyia pointi 7. Ashanti United ilimaliza bila pointi.

Simba na Yanga zitapambana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro huku zikiwa tayari zimepata tiketi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa mwakani. Hakuna donge nono lillilotangazwa kwa mshindi kufuatia ligi hiyo kukosa mdhamini.

Tutazidi kujuzana yale yatakayojiri kabla ya Jumapili.

3 comments:

Anonymous said...

Tunaombeni mikakati ya jinsi ya KUIFUNGA SIMBA SAFARI hii maanake tumechoka kufungwa na hawa watani wetu kila kukicha !!!

Anonymous said...

Ligi ndogo ina maana kuna ligi nyingine au ndo ligi ya mwaka huu imeisha hivyo???

CM said...

Msimu mpya wa ligi utaanza Agosti 2007 hadi Mei 2008.

Ligi ndogo ilikuwa kwa ajili ya kipindi hiki cha mpito ambapo TFF inaelekea kwenye kubadili kalenda yake ili iende sawa na nchi za Ulaya na baadhi ya nchi za Afrika kama Misri, Afrika ya Kusini n.k

Kwa maelezo zaidi kuhusu ligi ndogo ilivyokuwa hebu cheki hii posti yangu ya tarehe 28 Machi 2007

http://yangatz.blogspot.com/2007/03/utetezi-kuanza-kwa-moro-utd.html