Friday, July 06, 2007

Victor Mwandike kuamua pambano

Mwamuzi Victor Mwandike ndiye atakayeamua pambano la fainali la watani wa jadi, Yanga na Simba Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Tayari Simba wamepinga kuchezeshwa na mwamuzi huyo kwa madai kwamba Mwandike amekuwa akiipendelea sana Yanga na pia wamedai kwamba michezo mingi anayochezesha inakuwa na maamuzi yenye utata.

Waamuzi wasaidizi ni Soud Abdi na Zuhura.

Wenzetu wameingiwa na mchecheto, labda wanatutisha tu ili tuvimbe vichwa tujue kwamba mwamuzi ni wetu. La muhimu ni kucheza kwa kufuata sheria 17 za soka pamoja na kuonyesha fair play.


6 comments:

Anonymous said...

Jamani mechi kubwa kama hii hakuna anayetoa maoni? Mie nawatakia kila la heri vijana wetu.

Anonymous said...

Dakika ya 60, Yanga 1 - 1 Simba

Tutazidi kufahamishana. Simba wamepata bao lao dk. ya 2 kwa penalti na Yanga tumesawazisha dk kama ya 55 hivi, bao likufungwa na Said Maulid.

JM

Anonymous said...

Dakika 90 zimemalizika, matokeo:
Yanga 1 - 1 Simba

Zitaongezwa dakika 30, maana mshindi lazima apatikane.

JM.

Anonymous said...

Tumeshindwa kwa matuta.

Anonymous said...

Yes, imekuwa bahati mbaya tumepoteza ubingwa kwenye penalti. Hata hivyo vijana wamejitahidi.

Tujipange upya kwa msimu ujao, na mashindano ya kimataifa mwakani.

JM.

Anonymous said...

Ndugu zangu ni kweli inauma lakini hatujapoteza vyote. Bado tuna tiketi yetu ya kombe la Shirikisho Afrika.

Ligi mpya itaanza mwezi ujao. Ni wakati wa kuangalia tumejikwaa wapi. Mungu ibariki Yanga

CM