Monday, July 09, 2007

All is not gone

Wadau poleni sana kwa msiba wa kupoteza ubingwa wa Tz Bara. Ni kweli inauma kufungwa na watani zetu wa jadi Simba lakini alichopata Simba ni nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika lakini na sisi tuna nafasi yetu kwenye kombe la Shirikisho Afrika.

Hatuwezi kuwalaumu wachezaji waliokosa penalti jana katika pambano la fainali kwani katika matuta, lolote linaweza kutokea. Hata hao Simba si wataalam sana wa matuta kwani mapema mwaka huu walitolewa na Texile de Pungue ya Msumbiji kwa njia hii hii ya matuta.

Tujipange upya kwa Kombe la Tusker na msimu mpya wa ligi utakaoanza mwezi ujao.

Mwisho kabisa katika hali ya ki-uanamichezo, tunawapongeza Simba kwa ushindi wa hapo jana.

Yanga Daima mbele, tusikate tamaa.


No comments: