Tuesday, July 10, 2007

Eti Micho kakimbia....Maximo je?
Vyombo mbalimbali vya habari leo vimeripoti kwamba kocha mkuu wa Yanga Milutin Sredojevic 'Micho' ametimka nchini na hatarejea katika klabu hiyo.

Hata hivyo gazeti moja la michezo lilimnukuu Micho akisema kwamba anakwenda kwao Serbia kutibiwa kwani hali yake si nzuri na amepoteza takriban kilo 7 baada ya ugonjwa wa tumbo ulioikumba timu hiyo huko Arusha hivi karibuni.

Tunachojiuliza hapa ni kwamba mtu ukienda nyumbani kupumzika baada ya ligi ndiyo unakuwa umeondoka moja kwa moja? Mbona Marcio Maximo amerudi kwao Brazil kupumzika? Ina maana na yeye hatarudi?

Jambo jingine ambalo limekuwa likizungumzwa ni juu ya kocha huyu (Micho) kujiunga na Supersport United ya Afrika ya Kusini. Tayari Supersport imemteua Gavin Hunt kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo mara tu ligi ya nchi hiyo ilipomalizika mwezi wa 5 mwaka huu ili ashike nafasi iliyoachwa wazi na Pitso Mosimane. Kwa hali hii nafasi ya Micho kwenye klabu hii ya huko Sauzi haipo.

Tuvute subira, tunaamini kwamba bado tupo na Micho.


4 comments:

Anonymous said...

Magazeti ya bongo always yanaandika habari za kuuzia magazeti. na kama tukifuatilia kila kinachoandikwa basi tutaugua magonjwa ya moyo...!

Kumbuka hata mwezi ulopita Micho alipokwenda Uganda na Ethipia kutafuta wachezaji wa kuongeza nguvu Yanga, magazeti yaliandika kuwa amekwenda kusaini mikataba na vilabu vya huko. Ni rahisi kwao kuandika habari ya uongo na kuuza gazeti, kuliko kuifanyia utafiti habari kabla ya kuandika.

Micho mwenyewe amesema hata kama Yanga ingeshinda mechi ile bado angeondoka tuu kwenda kupumzika, na hakuna wakati muafaka mwingine zaidi ya sasa ambapo hatuna mashidano... kocha na wachezaji wapewe mapumziko, ili maadalizi ya ligi mpya yakianza kila mtu awe fresh...

Ni hayo tuu kwa sasa,

JM.

kifimbocheza said...

Mie sina shaka, Micho hatatuacha kwenye mataa. Yupo sirioz.Pia, baada ya kutembelea wenzetu pale jangwani wiki kadhaa zilizopita, nimeona kiasi wanachama wanampenda.

Yanga Bolje!!

Anonymous said...

Magazeti ya Tanzania yanashangaza sana. Alipoenda Uganda kuna magazeti yaliandika kuwa hatarudi, lakini aliporudi hayakuandika kitu. Yaliamua kukaa kimya. Haya ni matumizi mabaya ya uhuru wa kuandika na pia ni kukosa objectivity.

Anonymous said...

Mdebwedo tu hamna lolote.