Wednesday, July 11, 2007

Tusker Challenge Cup
Michuano ya kila mwaka ya Tusker Challenge Cup inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu ambapo vigogo Yanga na Simba ni miongoni mwa timu zilizoteuliwa kushiriki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF jana, ukiacha vigogo hao, timu nyingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni mabingwa watetezi Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kwa upande wa Tanzania, SC Villa ya Uganda na Tusker FC ya Kenya.

Mshindi wa michuano hiyo iliyopangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 28 hadi Agosti 11 atajinyakulia kitita cha sh. milioni 25, mshindi wa pili milioni 10 na mshindi wa tatu ataondoka na sh. milioni 5.

Ni nafasi sasa ya Yanga kufanya kila jitihada kunyakua kitita hicho na uzuri zaidi utakuwa kwa kumfunga Simba kwenye fainali. Yote yanawezekana.

Yanga haijawahi kubeba taji hilo tangu lilipoanzishwa mwaka 2002.

No comments: