Saturday, July 14, 2007

Tunao SC Villa na Mtibwa Sugar katika Tusker


Yanga imepangwa kundi moja na SC Villa ya Uganda pamoja na Mtibwa Sugar katika michuano ya Kombe la Tusker 2007 itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzi Julai 28.

Ratiba hiyo inaonyesha kwamba Yanga itaanza michezo yake tarehe 29 Julai kwa kupambana na SC Villa na mechi yake ya pili itakuwa tarehe 5 Agosti kwa kuumana na Mtibwa Sugar. Timu hizi tatu zipo katika kundi B.

Kundi A lina timu za Simba, Kagera Sugar na Tusker ya Kenya.

Ratiba kamili ni kama ifuatavyo:

MAKUNDI
Julai 28: (Kundi A) - Simba vs Tusker
Julai 29: (Kundi B) - Yanga vs SC Villa
Julai 31: (Kundi A) - Kagera Sugar vs Tusker
Agosti 1: (Kundi B) - Mtibwa Sugar vs SC Villa
Agosti 4: (Kundi A) - Kagera Sugar vs Simba
Agosti 5: (Kundi B) - Yanga vs Mtibwa Sugar

NUSU FAINALI
Agosti 7: Mshindi "A" vs Mshindi wa pili "B"
Agosti 8: Mshindi "B" vs Mshindi wa pili "A"

MSHINDI WA TATU
Agosti 10: Walioshindwa kwenye Nusu Fainali

FAINALI
Agosti 11: Walioshinda kwenye Nusu Fainali
Mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh mil. 25, wa pili sh. mil. 10 huku wa tatu akiambulia sh. mil. 5.

Mchezaji bora wa michuano hiyo, atapata sh mil. 1 huku timu yenye nidhamu ikipata sh mil 2.

Kazi ipo.


No comments: