Wednesday, July 18, 2007

Maneno maneno tu!!!!!

Wapenzi wadau samahani kwa kutotuma kitu kwa muda kidogo hii ni kwa sababu hakuna taarifa za uhakika kutoka kwenye klabu yetu.

Kwa muda sasa yamekuwa ni maneno maneno tu mitaani. Mengi yanayozungumzwa ni:

  • Kurejea au kutorejea kwa Kocha wetu Micho ambaye amekwenda kwao Serbia na tangu amekwenda huko hajawasiliana na klabu.
  • Kuongezwa kwa washambuliaji nguli Ben Mwalala kutoka Kenya na Abeid Mulenda kutoka DRC ili kuongeza nguvu katika michuano ya Tusker 2007.
Hayo ni kwa uchache yaliyotawala mitaani lakini si taarifa rasmi kutoka katika klabu.

Lakini wadau tunaweza pia kuchangia kuhusu kuongeza washambuliaji. Je hao waliotajwa ni vema waongezwe?5 comments:

Anonymous said...

Naunga mkono kuongezwa kwa Mwalala na Mulenda kwenye kikosi chetu. Kama tutakumbuka, toka alivyoondoka Mwalala na alipoumia Gulla, foward line yetu imethirika sana. Pamoja na heshima zote nilizonazo kwa washambuliaji wetu wa sasa Abuu, Mwaikimba na Moris, ni ukweli kuwa magoli yamekuwa adimu sana Yanga. Pia napendekeza kuwa SMG arudishwe kwenye wingi kama zamani na pia Mwalimu aangalie uwezekano wa kumtumia Abdi Kassim kama mshambuliaji badala ya kiungo wa kushoto. Hii ni kama tutashindwa kuwapata kina Mwalala. Naamini Mwaikimba anaweza improve akicheza na Abdi. Tatizo letu lingine ni kuwa kiungo wetu wa Mbele (Kyemba anacheza taratibu mno). Itakuwa vema kama tutampata Chuji halafu Kyemba acheze kushoto.

Anonymous said...

Naungana na Anonymous wa kwanza hapo juu. Ni kweli kuwa magoli ya uhakika yamepungua tangu aondoke Mwalala na Baraza. Kwa hiyo naamini tukipata washambuliaji nguli wawili ama watatu, tutafanya vizuri zaidi. Heshima zote kwa Kina Mourice na Mwaikimba, lakini nadhani wanastahili kupewa changamoto na kina Mwalala na wengineo.

Pia pengine tunaweza kuwa-release wachezaji ambao hawajacheza hata mechi moja hadi sasa (kina Lulanga na Swita) wakasajiliwe na timu zilizopanda daraja msimu huu kama Toto na Coastal Union. Nadhani huko watakuwa na msaada zaidi kuliko kuendelea kukaa benchi la Yanga.

JM.

Anonymous said...

Kweli magazeti yanaandika mengi, ila nimevutiwa na habari hii:

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/7/20/habari61.php

Hivi kuna mdau mwenye ukweli wa habari hii? Maana sijasikia habari za Kampuni tangu uchaguzi ulipoisha. Binafsi sipingi viongozi kuwa na misimamo tofauti, lakini nadhani kuna umuhimu wa kuweka mambo hadharani kwa wanachama/wapenzi.

Pia nadhani viongozi wa Klabu wanayo kazi kubwa, ya ku-mobilise wapenzi wote wawe wanachama na washiriki ktk maendeleo ya Klabu. Kwa hiyo wakipunguziwa mzigo wa timu, naamini watafanya mambo megine vizuri zaidi. After all, Kampuni iko chini ya Klabu, kwa hiyo indirectly bado wanakuwa na control kwenye timu.

Anonymous said...

Nimefanya mawasiliano na Katibu Mipango wetu ili akipata muda apite humu na kutoa mawazo yake.

CM

Anonymous said...

Tutashukuru sana kama atapata 'nafasi' ya kufika hapa na kutoa maelezo. Bila shaka Wadau watakuwa na mengi ya kumuuliza.

JM.