Wednesday, June 27, 2007

Tribute to Amina Chifupa


Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya Hayati Amina Chifupa ambaye amefariki dunia jana.

Amina alikuwa mpenda michezo na miongoni mwa mambo ambayo atakumbukwa ni ushiriki wake mkubwa katika kuwaendeleza vijana wadogo kwa kuwapa vifaa vya michezo na pia alikuwa mmoja wa wahamasishaji wakubwa wa timu yetu ya Taifa - Taifa Stars katika michezo yake miwili ya mwanzo ya kufuzu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, kundi la 7. Katika mechi ya kwanza dhidi ya Burkina Faso, alitoa zawadi ya 500,000/= kwa kila goli litakalofungwa na katika mechi ya pili, alisafiri na timu hadi huko Maputo, Msumbiji.

Sisi kama wanamichezo tunasikitika kupoteza kijana ambaye alikuwa ni mchango kwa Taifa katika kuendeleza michezo.

Mungu ailaze Roho ya Hayati Amina Chifupa mahali pema peponi.


No comments: