Thursday, June 14, 2007

Micho mkorofi au haeleweki?

Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Milutin Sredovedic 'Micho' ameingia katika minong'ono miongoni mwa wapenzi wa klabu ya Yanga kutokana na tabia yake ya kusimamisha wachezaji mara kwa mara.

Wachezaji ambao tayari wamewahi kukumbwa na sokomoko hilo kwa nyakati mbalimbali ni Yusuf Hamis, Edwin Mukenya, Lulanga Mapunda, Gaudence Mwaikimba, Emmanuel Switta na hivi karibuni Kocha wa makipa Razak Siwa.

Katika siku za hivi karibuni baadhi ya wachezaji pamoja na wapenzi wa Yanga wamelalmikia kitendo cha kocha huyo kwani kinawakosesha amani na wakitolea mfano kushuka kiwango kwa beki Yusuf Hamis huenda kimesababishwa na kocha huyo.

Hata hivyo mambo anayofanya Micho si ya mageni katika Ulimwengu wa soka. Hata Sir Alex Ferguson na makocha wengine wakubwa duniani wanatoa adhabu kwa wachezaji wanaokosa nidhamu. Kwa mawazo yangu naona nia ya kocha si mbaya kwa klabu, labda tu wachezaji wanatakiwa kuacha kuwa na mawazo kwamba bado wapo katika soka la ridhaa. Sasa hivi soka ni la kulipwa, hivyo wachezaji wanatakiwa kuonyesha uwajibikaji zaidi wanapokuwa ndani ya mkataba.


5 comments:

Jaduong Metty said...

Nadhani umegusia kitu ambacho kinafanya soka la Bongo liwe chini - nalo ni akili finyu. Lakini cha ziada umeongelea ukweli kwamba wachezaji ni kama vile ni wakulipwa. Kwa mantiki hiyo, kocha - ambaye ni kama kibosile wao- anajukumu la kuhakikisha nidhamu kwenye timu.

Micho anakuja na mtazamo na kapiriensi ka Ulaya, ambao unathamini na kuheshimu kazi. Tatizo tuna manazi ambao wana akili finyu, ambayo kwa kiasi kikubwa kimekuwa kikwazo kwa maendeleo ndani ya Yanga na klabu zingine Bongo.

Anonymous said...

Nimependa para yako ya mwisho. Bila wachezaji kubadilika ki-mtazamo, ni ngumu kwa wachezaji wetu kucheza Ulaya.

Ktk mpira wa kulipwa ambapo kila mchezaji anatamani kufika hasa Europe, Kocha (ama Manager) wa timu ndio bosi na mwajiri wa wachezaji. Mchezaji hata awe na jina kubwa kama Beckham au C. Ronaldo anajitahidi kuwa in good terms na kocha wake, maana ndio mwajiri wake. Adhabu anazotoa Micho kwa wachezaji zote anasema ni utovu wa nidhamu, na hilo sio siri, watanzania hatuheshimu kazi, sio mpirani tuu. Mtu yeyote ambaye ameshafanya kazi na boss toka Ulaya, atakwambia jinsi ufanyaji kazi wa wenzetu ulivyo. Kwao, kazi inakuja mbele ya kitu kingine chochote. Boss hategemei utegee kazi kwa sababu yoyote ile wakati ndio inakulipa mshahara.

Wachezaji wetu wamezoea kudekezwa hasa wakishapata jina kidogo. Anataka aje mazoezini siku na saa anayotaka mwenyewe. Mpira wa kulipwa hauko hivyo, namba yako unaifanyia kazi mwenyewe kwenye mazoezi.

JM.

NB:
Nina wazo lingine, halihusiani na hii topic moja kwa moja lakini naomba nilitoe tuu:

Kwanza ningependa kujua kama kuna mdau anafahamu kocha Jack Chamangwana amefikia wapi ktk kuanzisha timu za vijana klabuni?
Maana sijamsikia muda mrefu.

Pili ningependekeza zianzishwe timu za vijana kila mkoa, na kwa dar kila Wilaya. Timu hizi za under 10 na under 15 ziwe chini ya usimamizi ya matawi ya Yanga mkoani au wilayani. Jack anaweza kuzisaidia kwa kutoa program itakayofuatwa na makocha pamoja na kutoa mafunzo kwa makocha wa hizi timu.

Makocha wawe ni wachezaji wa zamani wa Yanga. Majuzi nilisikitika kusoma eti Peter Tino anaishi maisha ya kubahatisha leo hii, wakati wachezaji kama yeye ndo tunawataka wawafundishe vijana wetu namna ya kufunga mabao kama enzi zake..!

Wachezaji watakaotoka ktk hizi timu za vijana mikoani ndo waje kupewa mafunzo na Jack kwenye timu za under 15 na under 17. Baada ya hapo wanasajiliwa na Micho kwenye timu ya wakubwa wakifikia kiwango na wengine tunawauza nje ya nchi.

Bila shaka swali ni gharama za hizi timu:
Mfadhili wa klabu aombwe kuchangia kama sh. milioni 500 kwa miaka 5 (Yaani milioni 100 kwa mwaka). Hizi anaweza kuzitoa kama mkopo. Nina uhakika baada ya miaka 5 ya hii investment, Yanga itaweza kuuza wachezaji kadhaa nje ya nchi kwa kati ya million 20 - 50 kila mmoja. Fedha zinatakazopatikana ziende kulipa deni. Na Yanga itafaidika kwa kuwa na ushindani mkubwa wa namba na wachezaji walioandaliwa vizuri toka utotoni.

Wadau mnaonaje?

Jaduong Metty said...

@Anony 9:00AM
Nadhani wazo lako la kuwa na timu ya vijana ni zuri, lakini "umechemka" kidogo ulipotoa wazo la "mfadhili" wa timu kutoa pesa za kugharimia hii programu.

Kwa mtazamo wangu, Yanga ina uwezo wa kutengeneza pesa yenyewe bila ya kumtegemea mdosi yeyote. Ni suala la kuanza na mabadiliko ya kifikra na kutambua kwamba Yanga ina "brand name" kubwa kuliko Vodacom au IPP.

Ni suala la WanaYanga kujipanga na kuacha fikra za 1962!

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe kabisa Jaduong Metty. Well, kutumia mfadhili was just an example kuonesha numbers. Lakini naamini mtaji mkubwa wa Yanga ni mamilioni ya wapenzi wake, ambao wakiwekewa mpango mzuri wanaweza 'kuwekeza' ktk timu za vijana na kufurahia matunda yake baadaye.

JM.

Jaduong Metty said...

@JM
Hivi una contact zozote za viongozi wa Yanga tuanze kuwapa maarifa na ushauri wa bure?

Naami kwamba Yanga inaweza kuchukua ubingwa wa Afrika, lakini mambo lazima yabadilike kifrika kwanza kwa viongozi. Kwa sababu viongozi ndio wanasajili wachezaji, kubadilika kwa kifrika kutasaidia kuwapata wachezaji wanaolewa "vision" ya uongozi.

Nadhani kwamba kocha Maximo amewafumbua waTanzania macho kwamba timu siyo lazima iwe na majina makubwa, bali wachezaji wanaoelewa majukumu yao na "attitude" endelevu.

Nadhani viongozi wa Yanga wanahitaji sana semina.