Saturday, June 23, 2007

Uwanjani na Mtibwa leo

Mabingwa watetezi wa ligi ya Tanzania Bara, Yanga leo inaingia katika Uwanja wa Sheikh Amri Abied huko Arusha kupambana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi ndogo ya TFF hatua ya sita bora katika kundi A.

Kundi A lina timu tatu; Yanga Mtibwa Sugar na JKT Ruvu.

Yanga inatakiwa ishinde mchezo huo ili kujiweka pazuri mapema katika michuano hiyo ya kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa mwakani.

Katika kundi B lenye timu za Simba, Ashanti United na Polisi Morogoro zitacheza mechi zake katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na katika mechi ya ufunguzi wa kituo hicho, SImba itapambana na Ashanti United.

Kila la heri vijana wa Jangwani katika ligi ndogo hatua ya sita bora.


2 comments:

Anonymous said...

matokeo vipi?

Anonymous said...

Yanga 3 - 2 Mtibwa
Simba 2 - 1 Ashanti