Friday, July 27, 2007

Hawana lolote, Wametukimbia!

Wale wanaojiita 'Mabingwa wa kihistoria' wa michuano ya Tusker, Simba wamejitoa katika michuano hiyo ya mwaka huu baada ya kushindwa kuthibitisha ushiriki wao ndani ya muda waliopewa na TFF.

Awali Simba ilidai kwamba haitaweza kushiriki katika michuano hiyo endapo itafanyika Morogoro mpaka ipewe sh. milioni 5 kila mechi katika michezo yake miwili za mwanzo. Inasemekana kwamba mwamko wa mashabiki wa Morogoro kuhudhuria mechi si mkubwa sana na kwa kuliona hilo, TFF kwa kushirikiana na wadhamini wa michuano hiyo wakahamishia michuano hiyo Mwanza ambapo mashabiki wa huko wanajulikana kwa kujitokeza kwao kwa wingi kuangalia soka katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Tunachojiuliza hapa, hivi ni kweli hawa jamaa wamejitoa kwa vile gharama ni kubwa kama michuano itafanyika Mwanza? Wachezaji wao wenyewe wamesikitishwa na kitendo hicho ambacho kitawakosesha mengi ikiwemo nafasi ya kuonekana, kwani kocha wa timu ya Taifa Marcio Maximo alitaka kuitumia michuano hii kuangalia uwezo wa wachezaji ambao wanaweza kuongezwa kwenye kikosi hicho.

Kitendo cha kujitoa Simba ni cha kibinafsi zaidi, kwani waliona wakiingiza mguu katika michuano hii tutawafunga mabao mengi sana kwa jinsi tulivyojiimarisha. Viongozi wa Simba wamejifikiria wenyewe kwamba hivi sasa wanataka kuendeleza furaha yao ya kuifunga Yanga lakini walichofanya ni kuahirisha tu kifo.

Sasa sijui na kwenye ligi watatukimbia?

No comments: