Monday, July 30, 2007

Sare na SC Villa

Yanga imetoka sare ya 0-0 na SC Villa katika mchezo wa kwanza wa mchezo wa Kombe la Tusker uliofanyika jana katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Yanga ambayo ilimchezesha kwa mara ya kwanza mchezaji Athumani Iddi ilionekana kutokuwa makini hasa katika ufungaji.

1 comment:

Anonymous said...

Wadau,

Hivi nini hasa suluhisho (solution) la tatizo la ushambuliaji ktk timu yetu? Mimi hili naliona kama tatizo la taifa zima, na sio Yanga tuu.

Maana hata wale washambuliaji tuliodhani wakim-replace Mwaikimba kwenye Taifa Stars mambo yangekuwa murua, bado hakuna aliyefunga goli hata moja, so far.

Nadhani kuna umuhimu wa kuimarisha timu za vijana (watoto) na pia kuwatumia watu ambao waliwahi kufanya mambo makubwa enzi zao kama kina Peter Tino and the Manara's wawafundishe watoto namna wa ku-shoot accurately golini.

Maana huwa nashindwa kuelewa striker akipata chances 4 yeye na golikipa asifunge hata moja, utamfundishaje akuelewe...?

Nakaribisha maoni yenu..

JM.